Waasi wa Tuareg wapata ushindi Mali
By Maganga Media - Apr 2, 2012
Waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchini Mali wamesema wameuteka mji muhimu wa Timbaktu Kaskazini mwa nchi hio. Wakati hayo yakijiri, viongozi wa kijeshi waliofanya mapinduzi ya serikali wamesema wanarejesha utawala wa kikatiba na taasisi za nchi hiyo. Hii ni kutokana na agizo walilopewa na ECOWAS kuwa hadi leo wawe wamerejesha utawala wa kiraia ama wakabiliwe na vikwazo vya kiuchumi kutoka nchi jirani. Wanajeshi hao walichukua hataumu za uongozi siku kumi zilizopita.
Huko kaskazini, bendera ya waasi inapaa nje ya nyumba ya gavana wa Timbaktu, hatua hii inamaanisha kuwa miji yote muhimu kaskazini mwa Mali sasa iko chini ya mikono ya waasi wa Tuareg. Waasi hao sasa wanasema kuwa wako tayari kutangaza eneo huru ambalo wataliita Azawad. Lakini sio wao tu wanaojitangazia ushindi, kundi la wapiganaji wa kiislamu walio na lengo la utangaza utawala unaozingatia sheria za kiislamu nalo pia linajivunia ushindi huo. Imekuwa vigumu kuelewa jinsi makundi haya mawili yatagawana mamlaka.
Na katika mji mkuu Bamako, viongozi wa mapinduzi wametangaza kuwa wataunda serikali ya mpito ambayo itaandaa uchaguzi ulio wa huru na haki. Licha ya tangazo hilo nchi jirani huenda zisilegeze shinikizo dhidi ya waasi hao hadi watakapo tangaza ratiba yao ya kuondoka mamlakani.
Atakae twaa uongozi nchini Mali atakua amerithi matatizo makubwa zaidi ya hali ilivyokuwa awali, ikiwemo suala la waasi waliojitangazia eneo lao huru. Lakushangaza wanajeshi waliofanya mapinduzi walidai sababu yao kuu ya kuipindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure kwa kuwa alisihindwa kuzuia harakati za waasi wa Taureg kaskazini mwa nchi hiyo
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII