NDUGAI mgeni rasmi Tamasha la Pasaka Dodoma
By Maganga Media - Apr 2, 2012
Naibu spika Job Ndugai (MB wa Kongwa) |
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ndiye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka litakalofanyika Jumatatu ya Pasaka Aprili 9 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alisema Ndugai amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo Dodoma.
Mbali na Ndugai, tayari Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
"Napenda kuwaambia kwamba Ndugai amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Pasaka litakalofanyika Dodoma na atashirikiana na Wakristo kusherehekea tamasha hilo kwenye Uwanja wa Jamhuri," alisema Msama.
Msama alimshukuru Ndugai kwa kukubali mwaliko wa kuhudhuria tamasha hilo la Pasaka lililolenga kuchangia watoto yatima na kusaidia wajane wasiojiweza. Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.
Akizungumza kuhusiana na tamasha hilo, Ndugai ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, alitoa mwito kwa wakazi wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo. Ndugai alisema Msama Promotions imesaidia vijana, wajane na yatima kupitia tamasha hilo, hivyo ni vizuri kwa wakazi wa Dodoma na Singida kuiunga mkono kampuni hiyo kwa kuingia kwa wingi katika tamasha hilo Jumatatu ya Pasaka.
Wasanii wa nyimbo za Injili watakaopamba tamasha hilo ni Rebecca Malope, Rose Muhando, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration, kwaya ya Kinondoni Revival na Mwinjilisti Faraja Ntaboba
Wasanii wa nyimbo za Injili watakaopamba tamasha hilo ni Rebecca Malope, Rose Muhando, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration, kwaya ya Kinondoni Revival na Mwinjilisti Faraja Ntaboba
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII