Roketi ya Korea Kaskazini yaanguka
By Maganga Media - Apr 4, 2012
Habari kutoka Japan, Korea Kusini na Marekani zinasema kuwa mpango wa Korea Kaskazini wa kurusha angani roketi umeshindwa.
Roketi hiyo ilitazamiwa kupaa angani katika hatua tatu, kuelekea Kusini kutoka eneo ilikorushiwa, kupitia ufuo wa Magharibi wa Korea na kupita katikati mwa kisiwa kilichoko katikati mwa Taiwan na Japan cha Okinawa, kabla ya kuanza sehemu yake ya pili ya kupaa angani karibu na Ufilipino.
Lakini vyombo vya habari vya Marekani vinasema kuwa kulikuwa na mwanga mkubwa zaidi baada ya roketi hiyo kuwa sekunde 90 angani, na msemaji wa jeshi la Korea Kusini alisema kuwa urushaji huo wa roketi umefeli. Alifafanua kwamba kombora hilo lilikatika vipande viwili na kuanguka chini.
Licha ya kutofualu kwa urushaji huo wa roketi angani ni wazi kuwa watu wengi watashutumu jaribio hilo.
Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa limetangaza kuwa litakuwa na kikao maalumu hii leo na Rais wa Korea Kusini amesema kuwa maafisa wakuu wa usalama wataandaa kikao maaulu cha kujadili usalama nchini.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII