HABARI MPYA LEO  

Viongozi wa ECOWAS wasitisha safari Mali

By Maganga Media - Mar 29, 2012

Viongozi wa ECOWAS

Ujumbe wa viongozi wa Afrika Magharibi umeachana na mpango wake wa kwenda Mali kujadiliana na viongozi wa mapinduzi ya wiki iliyopita baada ya maandamano ya watu wanaounga mkono mapinduzi kuvamia uwanja wa ndege klatika eneo la kupaa na kutua ndege. Nchi jirani na Mali tayari zimeweka majeshi ya kulinda amani katika tahadhari tayari. 

Waandamanaji  nchini Mali
Jumatano maelfu ya watu waliandamana mitaani kuunga mkono mapinduzi hayo. Wengi walikasirishwa na kile wanachokiita kuwa ni ‘kuingiliwa mambo ya ndani na wageni’ "Viongozi wa mapinduzi wanatakiwa kutatua matatizo kaskazini,ufisadi na elimu. Hayo ni muhimu kuliko uchaguzi. " Mmoja wa waandamanaji, Khalifa Sogo, aliliambia shirika la habari la Reuters.

Kuhusu suala la katiba Mpya

Viongozi wa mapinduzi wametoa maelezo ya katiba mpya pamoja na kutangaza tarehe ya uchaguzi ambapo wale waliohusika na mapinduzi hawataruhusiwa kushiriki ingawa tarehe halisi haijatangazwa bado.
Mapinduzi yaliongozwa na askari ambao hawakufurahishwa na jinsi serikali ya Bw Toure ilivyokuwa ikishughulikia suala la waasi wa Tuareg kaskazini mwa nchi. Waasi wa Tuareg wameliviondoa vikosi vya jeshi katika miji kadhaa ya kaskazini katika miezi ya hivi karibuni.

Chini ya katiba mpya kamati ya mpito yenye wajumbe 26 kutoka vikosi vya usalama na raia 15 watashirika madaraka. Wale watakaofanya kazi katika kamati hiyo wamepewa kinga ya kushtakiwa. Baadhi ya nyaraka katika katiba hiyo zinafanana na katiba ya sasa yaMalizikiwemo uhuru wa kujieleza, mawazo na kutembea.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII