HABARI MPYA LEO  

KESI YA KUPINGA USHINDI WA SERUKAMBA YAFUTWA

By Maganga Media - Mar 29, 2012

MBUNGE WA KIGOMA MJINI ( C.C.M)Mh PETER SERUKAMBA
Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tabora Stella Mugasha amefuta kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Ubunge, iliyokua inamkabili mbunge wa jimbo la Kigoma mjini Peter Serukamba, kutokana na upande wa madai kukaidi amri ya mahakama kwa kushindwa kupelea mashahidi.

Mwanzoni mawakili wa upande wa mdai ambae ni Ally Mleh  walijitoa katika kesi hiyo kwa kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, na hivyo mlalamikaji kuomba apewe muda wa kutafuta mawakili wengine lakini alishindwa huku akipinga kesi hiyo kuendelea kusikilizwa na jaji Mugasha.

ALIYEKUWA MGOMBEA WA CHADEMA

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII