Wafanyakazi nchini Hispania wapinga serikali kubana matumizi
By Maganga Media - Mar 30, 2012
Maandamano ya wafanyakazi nchini Hispania |
Maelfu ya wafanyakazi nchini Uhispania wanashiriki mgomo wa nchi nzima kushinikiza serikali kutoendelea na mpango wake wa kubana matumizi zaidi ya fedha kwa lengo la kukabiliana na mdororo wa kiuchumi. Mgomo huo ambao umeanza toka jana umeshuhudia huduma mbalimbali nchini humo zikisimama ikiwemo viwanja vya ndege kufungwa, shule pamoja na vyuo kufuatia wafanyakazi wa huduma hizo kushiriki kwenye mgomo huo wa nchi nzima.
Mgomo huo ni mtihani wa kwanza kwa waziri mkuu mpya Mariano Rajoy ambaye ametangaza serikali yake kuchukua hatua zaidi za kubana matumizi kwa lengo la kukabilina na madeni ya ndani na kupunguza matumizi ya serikali.
Mwaka huu peke yake nchi ya Hispania inakabiliwa na changamoto ya raia wake wengi kukosa ajira ambapo taasisi za utafiti wa ajira zimerekodi zaidi ya 23 ya wananchi wa hispania hawana ajira kikiwa ni kiwango cha juu zaidi barani Ulaya.
Shirikisho la wafanyakazi nchini humo limesisitiza kuendelea na mgomo huo iwapo serikali ya Rajoy haitasikiliza kilio cha wafanyakazi ambao wanataka nyongeza ya mshahara na maslahi bora kazini.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII