HABARI MPYA LEO  

NAFASI ZA MASOMO MWAKA 2012/2013 WIZARA YA AFYA

By Maganga Media - Mar 26, 2012

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2012/13 

Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 April, 2012. 

1. Kozi zinazotangazwa ni: 

A. Kozi za ngazi ya Stashahada:

(i) Afisa Afya ya Mazingira (Health Officer)
(ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)
(iii) Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)
(iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)
(v) Optometria (Optometry)
(vi) Tabibu (Clinical Officer)
(vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)
(viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)
B. Kozi za ngazi ya Cheti
(i) Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)
(ii) Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)
(iii) Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)
(iv) Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)
C. Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa ‘Distance Learning)
(i) Kozi ya Tabibu
2. Muda wa Mafunzo:
(i) Miaka mitatu (3)kwa kozi za Stashahada
(ii) Miaka miwili (2) kwa kozi za Ngazi ya cheti

3. Sifa za Muombaji:

Waombaji watarajali (Pre-service):
(i) Awe raia wa Tanzania
(ii) Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2007 na kuendelea
(iii) Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia kwa kozi za Stashahada . Maksi hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.
(iv) Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia na Fizikia. Maksi hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(v) Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua E, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(vi) Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.

Waombaji wa wanaojiendeleza (In-service) kuchukua Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya Masafa - Distance learning:

(i) Awe amemaliza kidato cha nne
(ii) Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Waganga Wasaidizi Vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.
(iii)Awe na barua ya mwajiri wake
Waombaji katika kipengele hiki watatakiwa kuchukuwa ‘Bridging course’ kwa miezi 9 na
kufaulu, ndipo waweze kuendelea na masomo ya Tabibu.

4. Utaratibu wa kutuma maombi:
(i) Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, waganga wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya wizara. Pia ipo kwenye mtandao - website ya wizara ya Afya www.moh.go.tz
(ii) Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, itawasilishwa pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).
(iii)Malipo yaingizwe kwenye akaunti ,Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC CORPORATE BRANCH.
(iv) Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti ya malipo ya Benki, inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.
(v) Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.
(vi) Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.
(vii) Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa wakuu wa kanda kulingana na eneo ambalo muombaji alipo. Kanda ya Mashariki itakuwa na sehemu tatu za kupokelea (No. a, i na j. Anwani za wakuu wa kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-

a) Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii S.L.P. 1060, Morogoro - (EZ)
b) Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma - (WZ)
c) Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara) Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara - (SZ)
d) Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga) Chuo cha Mafunzo ya Walimu wa Afya, S.L.P.1162, Arusha - (NZ)
e) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya - (SWHZ)
f) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa) Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa - (SHZ)
g) Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) Chuo cha Uuguzi, S.L.P. 595, Dodoma - (CZ)
h) Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza - (LZ)
i) Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam - (EZI)
j) Mkuu wa chuo cha Tabibu, S.L.P. 30282, Kibaha - (EZK)

Mwombaji ajaze kwenye fomu ya benki kanda/chuo ambayo atapeleka fomu zake kwa kujaza herufi zilizo ndani ya mabano hapo juu, zilizoandikwa mwisho kabisa wa anuani ya kila kanda. Herufi hizo zijazwe upande wa kushoto wa fomu ya benki wakati mwombaji wanajaza mambo mengine kwenye fomu. Fomu zitapokelewa kwenye vyuo vilivyoainishwa hapo juu tu.

5. Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
a) Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya wizara na mbao za matangazo wizarani na Kanda za Mafunzo.
b) Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.

6. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2012.

7. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2012.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
Dar es Salaam.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII