Jalada la Dk Mwakyembe mahakamani utata mtupu
By Maganga Media - Mar 14, 2012
MKURUGENZI wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi, amesema hadi sasa ni vigumu kufahamu atakapopeleka mahakamani jalada la kesi kwa watu wanaotuhumiwa kutoa taarifa kwamba ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, unatokana na kulishwa sumu. “Ni vigumu kusema ni lini itapelekwa mahakamani... bado tunalifanyia kazii," alisema Feleshi akisisitiza uchunguzi wao ukikamilika wataamua kuipeleka mahakamani au la, kulingana na kanuni na taratibu za ofisi hiyo.
Jalada hilo lilifika kwa DPP likitoka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ambaye alisema uchunguzi wa polisi umebaini Dk Mwakyembe hajaugua kwa sababu ya kulishwa sumu, hivyo waliohusika kutoa kauli hizo watawachukulia hatua.
Jalada hilo lilifika kwa DPP likitoka kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ambaye alisema uchunguzi wa polisi umebaini Dk Mwakyembe hajaugua kwa sababu ya kulishwa sumu, hivyo waliohusika kutoa kauli hizo watawachukulia hatua.
Hata hivyo, Feleshi alisema kitendo cha kutopeleka moja kwa moja kesi hiyo haina maana wanamdharau Kamishna Manumba, bali wanatekeleza taratibu zao. Kwa sababu hiyo, Feleshi alisema wanachofanya wao ni kutekeleza utaratibu wao ndiyo utakaotoa picha halisi ya ama kupeleka kesi mahakamani au la. Feleshi alisema suala hilo linafanyiwa uchunguzi hasa ikizingatiwa Dk Mwakyembe, anaendelea na matibabu nchini India.
Feleshi hakuweka bayana majina yaliyopo kwenye jalada hilo alilopelekewa na DCI, lakini baadhi ya watu ambao waliwahi kuzungumza hadharani kwamba ugonjwa wa kiongozi huyo unatokana na kulishwa sumu, ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta. Ripoti ya uchunguzi aliyoisoma Manumba Februari 16, mwaka huu Dar es Salaam, alisema inaonyesha Dk Mwakyembe hakulisha sumu.
Kwenye uchunguzi huo ambao pia alisema ulijumuisha taarifa kutoka hospitalini India ambako Dk Makyembe alikuwa anatibiwa, unawapa picha kuwa waliosema taarifa hizo hadharani wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Ripoti ya DCI ilizua utata na maswali mengi, huku Dk Mwakyembe akielezea kushangazwa na ripoti hiyo na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii haikuiunga mkono.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII