Chama Tawala cha zamani nchini Zambia (MMD) chafutwa kwa madeni
By Maganga Media - Mar 14, 2012
Ramani ya Zambia |
Chama tawala hapo zamani nchini Zambia cha MMD kimepokonywa hadhi yake ya kisheria kwa kushindwa kulipa ada inayohitajika na vyama vilivyosajiliwa kwa kipindi cha miaka 20 takriban dola $75,000 (£50,000).
Msajili wa mashirika amesema kua Chama hicho cha MMD kimefutwa kutoka daftari la usajili kwa kushindwa kulkipa ada chini ya sheria.Chama hicho kimekanusha kua kinadaiwa na kusema kitakata rufaa kwa kile lililotaja kua shambulio dhidi ya demokrasi. Endapo uwamuzi huu utazingatiwa, chama cha MMD kitapoteza viti vyake katika bunge.
Hiki ni mojapo ya vyama vikongwe vya kisiasa kilichoingia madarakani mnamo mwaka 1991 katika uchaguzi wa kwanza ulioshirikisha vyama vingi.
Mwaka jana kilijitokeza kua chama kikubwa cha upinzani kikiwa na viti 53 na baada ya hapo kikashindwa na chama cha Patriotic front cha Rais Michael Sata aliyeshinda uchaguzi na kushika hatamu za uongozi wa Zambia.
Vyama vyote nchini Zambia vinawajibika kujiandikisha na msajili wa mashirika, taasisi ya serikali. Mkuu wa shirika hilo, Clement Andeleki,ameuambia mkutano wa wandishi wa habari mjini Lusaka kua amesimamisha usajili wa chama cha MMD kutokana na kukaidi sheria inayoyataka mashirika na vyama.
Aliongeza kusema kua uwamuzi huu ulifikiwa kama kitendo cha kipekee kuwasilisha ujumbe mzito kwa mashirika yanayokaidi sheria ya usajili.
Kumekuepo juhudi za kutaka deni ambalo MMD kinadaiwa zilipwe tangu mwezi Septemba ambapo Rais Sata alishika hatamu za uongozi.
Mwakilishi wa Chama hicho cha MMD wanatazamiwa kuomba uchunguzi wa kisheria ufanyiwe kuhusiana na uwamuzi huu, alisema msemaji wa MMD, Dora Siliya.
Msemaji huyo amesema kua chama chake kililipa kila pesa inayohitajika mapema mwezi Januari - ingawa hakikupokea majibu kuhusu suala hilo.Chama hicho kimekanusha kua kinadaiwa pesa yoyote.
Chama cha MMD kimepewa siku 21 kukata rufaa kupitia Wizara ya mashauri ya nchini.
Ikiwa chama hicho kitapoteza rufaa hio basi Spika wa bunge ana uhuru wa kutangaza nafasi zake za Bunge zimeachwa wazi - na kuamuru uchaguzi mdogo ufanywe ili kujaza nafasi hizo.
http://maganga-resources.blogspot.com
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII