HABARI MPYA LEO  

HESLB yatangaza walioshinda rufaa ya MEAN TEST

By Maganga Media - Mar 16, 2012

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu nchini (HESLB) imetangaza orodha ya majina ya wanavyuo wa Elimu ya juu nchini walishinda rufaa ya mean test walizokuwa wamepangiwa awali. Orodha hiyo iko katika makundi mawili la waombaji wapya 9wale wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea. Akitanagaza majina hayo, mkurugenzi wa bodi ya mikopo alisema kuwa hayo ni majina ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao walizoomba. 

Aidha, aliongezea kuwa, kutokana na ufinyu wa bajeti bodi ya mikopo imeshindwa kupitisha maamuzi juu ya wanafunzi wale ambao hawakupata kabisa mikopo kutokana na ufinyu wa bajeti au sababu nyingine kwa mwaka wa masomo wa 2011/2012. "Kwa taarifa hii, bodi inasikitika kuwataarifu wote waliokata rufaa na majina yao hayajaonekana kwenye hii orodha kujihesabu kuwa hawajafanikiwa.

BONYEZA LINK HAPA CHINI USOME ORODHA YA MAJINA

MWAKA WA KWANZA                                WANAFUNZI WANAOENDELEA
(First year students)                                    (Continuing Students) 

http://maganga-resources.blogspot.com

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII