HESLB yasisitiza kuwashitaki waliokaidi
By Maganga Media - Mar 16, 2012
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiriano, Cosmas Mwaisobwa |
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), inaendelea na uhakiki wa majina na vielelezo vitakavyotumika kuwapeleka mahakamani wadaiwa sugu waliokaidi kurejesha madeni yao ya mikopo waliyochukua wakati wanasoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiriano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema kwa sasa kinachofanyika ni ukusanywaji wa taarifa zitakazotumika katika ufunguzi wa kesi pamoja na mashitaka kwa wale wote ambao hawajarejesha madeni.
“Kwa sasa tunakusanya vielelezo vya kutosha, hatuwezi kukimbilia mahakamani pasipokuwa na udhibitisho wa kutosha, tunayakusanya majina pamoja na taarifa zao ili tuweze kuwafahamisha kuwa tunawafungulia mashitaka,” alisema Mwaisobwa. HESLB ilitoa notisi ya siku 21 kuanzia Januari 19, 2012 kwa wadaiwa wote wawe wamejitokeza na kufika ofisi za bodi. Kwa mujibu wa bodi hiyo, hadi sasa muda huo umeshapita na hakuna waliojitokeza, hivyo wameamua kuwafungulia mashitaka mahakamani.
http://maganga-resources.blogspot.com
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII