HABARI MPYA LEO  

Mfuko wa kusomesha yatima waanzishwa

By Maganga Media - Feb 28, 2012




MKUU wa Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara, Khalid Mandia, amesema wilaya imeanzisha mfuko wa elimu kwa kila mwananchi kuchangia Sh500 kwa kila mwaka.Mandia alisema mpango huo ni endelevu kwa kila kata kuchangia mfuko huo,  ili kusaidia kusomesha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi wenye uwezo wa taaluma.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu, Mandia alisema wamezipatia shule zote za sekondari magunia 150 ya mahindi kwa ajili ya chakula, hivyo kuwapunguzia mzigo wazazi.

Hata hivyo, Mandia alisema mahindi hayo yatachangiwa fedha kidogo kwa kila gunia kulipiwa Sh5,00 na kwamba, wanasubiri tani nyingine 700 ili baadhi zigawanywe kwenye shule zilizopatiwa mahindi pungufu.Kwa upande wake, Ofisa Elimu ya Sekondari Wilayani Simanjiro, Julius Mduma, alisema wilaya hiyo ina sekondari 15, kati ya hizo ni moja inayomilikiwa na mtu binafsi.

Mduma alisema kati ya wanafunzi 1,979 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wilayani humo, hadi sasa 1,093 wameripoti na 860 bado hawajaripoti.Alisema sekondari wilayani humo zina walimu 113 na kwamba, 34 wamekwenda kujiendeleza katika hatua mbalimbali za elimu na kwamba,  wengi wao ni walimu wa leseni na mwaka huu wamepokea wapya 44.

Katika kikao hicho wadau hao walitakiwa kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza, kutokana na wilaya hiyo iliyokuwa inashika nafasi ya kwanza mkoani humo kwa kufaulisha darasa la saba, mwaka jana ilishika nafasi
ya tatu.
Na gazeti lako la mwananchi
http://maganga-resources.blogspot.com

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII