HABARI MPYA LEO  

Kesi ya mauaji ya marehemu Steven Kanumba inayomkabili movie star wa Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kutajwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku suala la umri wa mshitakiwa huyo likiendelea kuwekwa kiporo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO, Wakili wa Serikali KENNETH SEKWAO amesema upelelezi bado haujakamilika na kwa sasa ipo katika hatua ya kutajwa.

Mapema baada ya LULU kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake STEVEN KANUMBA April mwaka huu, mawakili wanaomtetea waliwasilisha hoja ya kupinga umri wa mshitakiwa huyo na kutaka achukuliwe kama mkosaji mtoto kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 18 hali iliyolazimu suala hilo kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamua kulirejesha jambo hilo kwenye mahakama ya Kisutu.

Pamoja na kurejeshwa kwa suala hilo katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kumekuwa na ukimya wa muda sasa, kesi ya LULU imeahirishwa mpaka Disemba 17 mwaka huu ambapo itakwenda kwaajili ya kutajwa.

Hivi karibuni mwanamuziki wa kike wa nchini Tanzania, Rehema Chalamila aka Ray C amerejea nchini baada ya kukaa Nairobi, Kenya kwa zaidi ya mwaka mmoja.


Alipozungumza  hivi  karibuni  baada  ya kufika, mrembo huyo alisema anahitaji mume wa maana ambaye atamuoa.

“Sina mume wala mpenzi, kwa sasa nipo single, ukiniulizia ishu za zamani ntakushangaa kweli, vigezo ndiyo hivyo, kama kuna mtu yupo tayari ajitokeze tufunge ndoa,” alisema Ray C.

Aliongeza kuwa akimpata mume huyo yupo tayari kumzalia watoto wawili na amechoka na maisha ya usela na kuwa na mahusiano na watu maarufu.

Wanaume wa Kenya wamekisikia kilio chake na wamewasiliana na mtandao wa Daily Post wa Kenya kumwambia Ray  C watampa penzi moto moto.

“Ray C if u wish 2 huk up wit mi,take tiz no.0702868104, I’m in Thika central Kenya.”

“Hey somebody hook me up with the gal”

“She is a super hot chick !! What’s her email ? Lets hook up!”

“I am here to satisfy your needs”

“d.mokoro@yahoo.com.she can reach me, I also need a wife seriously”

“Rehema Chalamila contact me at danielluke76@gmail.com”

“Yes I can got me on diemoadish@gmail.com please”

“Come Baby come!”

“She is a very awesome lady n av always liked her. We all have past’s n it’s not something to keep on holding to … I am interested in her, to ask her out. I think she’s a good lady.”

“Ray C, if you come across this, reach me on wilnj85@gmail.com”

Katika hatua nyingine mtandao huo umesema kulikuwa na tetesi kuwa mhasibu wake nchini Kenya alimuibia pesa zake zote na hivyo akajikuta akishidwa kumudu maisha kwenye maeneo ya kifahari na hivyo kuhamia South B ambako alikuwa akiishi maisha ya kawaida.

Safari ya Prezzo nchini Nigeria imemrudisha bila kukipata kile alichokiendea baada ya Goldie kuonekana kutofurahishwa na ziara yake.


Prezzo aliyekuwa mshindi wa pili kwenye Big Brother Africa StarGame wiki hii alienda nchini Nigeria kuwaomba radhi wananchi wa huko na pia kutangaza nia ya kumfanya Goldie awe mke wake.

Katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Lagos, Prezzo alisema alienda nchini humo kumuomba uchumba Goldie.
Hata hivyo hakufanikiwa kuonana Goldie ambaye Prezzo alisema hakuwa anapokea simu yake.

Hadi leo Goldie hajazungumzia chochote kuhusu ziara ya Prezzo.

Shabiki mmoja kupitia Twitter alimuuliza Goldie “Good afternoon madam, is it true that Prezzo is in town?” na yeye kumjibu “I also heard the pope is catholic. Is it true?”

Baadaye aliandika, “Gone R d days wen a problem shared is a problem solved; nowadays a problem shared becomes a topic of discussion. So keep ur problems 2urself!”

Kisha kuongeza: “Any1 can say anything, after all talk is cheap. But it’s in ur ACTIONS dat we’ll C ur tru intentions&where ur heart lies.”

Baada ya muigizaji mkongwe Hashim Kambi kuanza kutayarisha filamu zake mwenyewe, Jackline Wolper naye ameunga tela.
Muigizaji huyo mrembo amesema kupitia kampuni ya JB Production, ataanza kuandaa filamu zake.

Katika azma hiyo, Wolper atasaidiwa na meneja wake Leah Mwendamseke aka Lamata.


Vyanzo vimedai kuwa tayari kampuni hiyo imekamilisha kurekodi filamu iitwayo Malipo ni Hatari.


“Nimeingia katika fani ya utayarishaji na kwa kuanza ninakuja na filamu ya Malipo, ni filamu ya kipekee kuanzia hadithi, waigizaji wake wameigiza katika kiwango kikubwa cha kimataifa , okay sisemi mengi bali mtaona katika filamu ya Malipo,” Jack aliuambia mtandao wa FC.


Miongoni mwa waigizaji walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Blandina Chagula ‘Johari’, Stanley Msungu ‘Seneta’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Mgata, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo, Slim na wengine.


Malipo ni Hatari imeongozwa na Lamata.


Mshindi wa pili wa Big Brother Africa Stargame Jackson Makini aka Prezzo yupo nchini Nigeria ambako ameenda kuwaomba radhi wananchi wa nchi hiyo.

Habari njema kwa mashabiki wake ni kuwa jamaa ana mpango wa kumuoa Goldie kama akilikubali ombi lake. Rapper huyo mwenye miaka 32 amesema hajasafiri kutoka Kenya hadi Nigeria ili kucheza tu bali kwenda kuelezea hisia zake kwa mwanamke ambaye Mungu aliwakutanisha naye kwenye jumba la BBA.

Katika mahojiano na waandishi wa habari nchini Nigeria, Prezzo, amewaomba radhi wanaijeria kwa namna alivyomfanyia Goldie mjengoni humo na kutangaza hadharani kuwa yupo tayari kufanya lolote ili amfanye Goldie mkewe.

‘I was not able to express all my feelings to Goldie in the house due to paranoia and I am ready to come and fight for a prize that worth it and that will make me a real winner…’ alisema Prezzo.

Tatizo ni moja. Goldie hapokei simu yake. Is it too late too little?
Diamond ameamua kutanua mabawa yake zaidi mwaka huu kwa kumshirikisha msanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria, J.Martins. Tayari amesharekodi sehemu zake kwenye wimbo huo kwenye studio za MJ Records chini ya producer Marco Chali.Habari zinadai kuwa kwa sasa wimbo huo upo kwenye hatua ya final mixing ambapo chorus ya wimbo huo imeimbwa na Diamond na dancer wake Mose Iyobo. Katika kuonesha kuwa bega kwa bega na madancer wake, Diamond ameamua kumpa shavu Mose ambaye ameonesha uwezo mzuri wa kuimba.

J.Martins ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani akichukua kozi maalum ya miezi mitatu ya masuala ya utayarishaji, tayari anausubiri wimbo huo ili aingize sauti yake.


Katika hatua nyingine  Diamond anaelekea mjini Washngton DC nchini Marekani kwaajili ya show. Kwenye safari hiyo Diamond anaenda na madansa wake wote wanne na msemaji wake.


Kwa mujibu wa Power Jams ya East Africa Radio, Diamond atafanya show kwenye mkutano mkubwa unaofanyika Marekani ambao wahudhuriaji wamemtaka akawape burudani.