HABARI MPYA LEO  

Watu 30 waachiliwa kwa dhamana Zanzibar

By Maganga Media - May 29, 2012

Watu thelathini waachiliwa kwa dhamana kufuatia ghasia mjini Zanzibar. Miongoni mwao ni pamoja na Viongozi wawili wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi wa Zanzibar kwa zaidi ya siku mbili. Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo ya kisiasa, kuachiwa kwa viongozi hao ambao walikuwa wanakabiliwa na kosa la kuandamana bila kibali kunaweza kukomesha uhasama wa takriban siku mbili baina ya wafuasi wa kundi hilo na polisi.


MABAKI YA JENGO LA KANISA LILILOCHOMWA MOTO KUTUATIA MACHAFUKO HAYO

Hali ilianza kuwa shwari mjini Zanzibar baada ya kuachiliwa kwa dhamana kwa wafuasi hao. Miongoni mwa waliopata dhamana hiyo ni Sheikh Mbaruku Saidi Khalfan na Musa Juma Musa wote wakiwa viongozi wa kundi hilo. Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Mwanakwerekwe majira ya saa nne asubuhi Jumatatu, baada ya kusomewa mashtaka ya kufanya mkusanyika haramu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, watuhumiwa hao kwa pamoja walikana tuhuma hizo.

Baadaye wakili wa watuhumiwa hao aliwaombea dhamana, ombi ambalo lilikubaliwa bila pingamizi lolote. Kukamatwa kwa viongozi hawa kumeleta sokomoto kubwa mjini Unguja hasa baada ya wafuasi wa kundi hilo kuamua kuandamana kwa lengo la kuishinikiza polisi kuwaachia. Hali iliyosababisha vuta nikuvute baina ya wafuasi hao na polisi ambao wamekuwa wakitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.

Uamsho ni kundi la kidini ambalo limejipa jukumu la kuwaelimisha wazanzibari kuhusu suala la muungano hasa wanapotoa maoniyaokatika Tume ambayo inakusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hata hivyo, taarifa zisizothibitishwa zinasema, kundihilolimejikita zaidi katika kuwahamasisha wananchi kuupinga muungano.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII