HABARI MPYA LEO  

Mlipuko wajeruhi 33 Nairobi Kenya

By Maganga Media - May 29, 2012

Polisi nchini Kenya inasema mlipuko uliojeruhi watu 33 katika mji mkuu Nairobi unaweza kuwa umesababishwa na bomu, baada ya hapo awali kulaumu hitilafu za umeme. Mlipuko huo uliharibu maduka katika barabara ya Moi Avenue wakati wa mchana. Mtu mmoja aliyeshuhudia alisema kifurushi kiliachwa karibu yake kabla ya mlipuko kutokea.
Massive blast rocks building housing several clothing stalls on Moi Avenue near the Mount Kenya University. Scores injured: deaths unclear
Thick smoke engulfs Mt Kenya University along Moi Avenue Street after an explosion rocked a city stal.At least 30 people have been injured in a 1:10pm explosion that rocked an exhibition stall next to Mt Kenya University Campus along Nairobi's Moi Avenue stree

Waziri Mkuu Raila Odinga amesema mlipuko huo unahusiana na magaidi. Mlipuko huo umesababisha bidhaa mbali mbali kama viatu, nguo na vioo vilivyovunjika kusambaa sehemu yote ya eneo hilo. Picha za Televisheni nchini humo zilionyesha watu wakikimbia mbali na majengo yaliyo karibu katikati ya mji waNairobi.

Awali Kamishna wa Polisi nchini Kenya Mathew Iteere, alisema huenda "hitilafu ya umeme" ndio chanzo cha mlipuko huo, kwa mujibu wa Televisheni ya NTV. Hata hivyo mlipuko huo unaiwekaNairobikatika hali ya wasiwasi. Kumekuwa na milipuko kadhaa hivi karibuni ndani na nje ya mji huo mkuu huku baadhi ikihusishwa na kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia kulikuwa na mlipuko mkubwa na huku vipande vipande vya vioo na vitu vingine vikiwarukia na kujeruhi watu waliokuwa karibu, Gazeti la Nation linaripoti.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII