Mkuu wa IMF alaumiwa!
By Maganga Media - May 28, 2012
Serikali ya Ufaransa imelalamika juu ya matamshi ya mkuu wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Christine Lagarde, ambayo yalionesha kuwa Wagiriki wanahepa kulipa kodi.
Mjini Athens, kiongozi wa chama cha kisoshalisti, Evangelos Venizelos, aliuambia mkutano wa kampeni za uchaguzi kwamba Bi Lagarde amewatusi wananchi wa Ugiriki. Mkuu wa IMF piya alisema kwenye mahojiano hayo, kwamba ana wasiwasi zaidi juu ya umaskini katika nchi za Afrika kusini ya Sahara, kushinda Wagiriki waliokumbwa na msukosuko wa kiuchumi.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII