Mapokezi ya Waziri wa Habari Na Naibu Wake
By Maganga Media - May 9, 2012
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifurahi na baadhi ya Watumishi mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Jengo la Golden Jubilee.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisaini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasali katika Ofisi za Wizara hiyo, anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Bw. Sethi Kamuhanda.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza kwa makini Mh. Waziri Dkt. Fenella Mukangara wakati alipokuwa akiongea na Uongozi wa Wizara hiyo.Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa Wizara Rose Bandisa,katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leornard Thadeo na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Bw. Clement Mshana.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisisitiza jambo kwa viongozi wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo (hawapo pichani) mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Amos Makalla.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akiongea na Uongozi wa Wizara hiyo (haupo pichani) mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo. (Picha Zote kwa Hisani ya WHVUM)
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII