HABARI MPYA LEO  

AWAMU YA PILI YA AIRTEL RISING STARS

By Maganga Media - May 11, 2012



Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Uzinduzi huo ulifanyika jana, Mei 10, kwenye Hoteli ya Sea Clif, jijini Dar es Salaam.



Mchezaji wa zamani wa Manchester United ya Uingereza Quinton Fortunewa pili kulia, akionyesha waandishi wa habari (hawako pichani) baadhi ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye michuano ya soka ya kimataifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars jana kwenye Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam. Kati ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technologia Mh. Professa Makame Mbarawa, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mashindano wa TFF Sandy Kawembe, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sam Elangallor na Mkurugenzi Bidhaa Airtel Afrika Obina Justine.


KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua awamu ya pili ya mpango wa kuibua na kusaka vipaji vya soka unaojulikana kama ‘Airtel Rising Stars’, zoezi lililoendeshwa na nyota wa zamani wa Manchester United, Quinton Fortune.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor, alisema mafanikio ya mwaka jana yanaonyesha mpira wa miguu, una uwezo wa kuunganisha makabila mbalimbali na pia kuleta hamasa kwa jamii, kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.
Alisema mwaka jana zaidi ya timu 11,000 Afrika, zilijiandikisha kushiriki kwenye michuano hiyo, kuanzia kwenye mtoano na kuchagua wachezaji ambao waliunda timu zilizoshiriki kwenye ngazi ya mkoa.
“Awamu hii ya pili, inafuatia ile ya kwanza ya mwaka jana kuwa na mafanikio makubwa. Lengo la mpango huu ni kuvipa vipaji vinavyochipukia chini ya umri wa miaka 17, nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kwa makocha waliobobea na pia kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao,” alisema.
Alisema kama ilivyokuwa kwa mwaka jana, mpango huu utaanzia ngazi ya mkoa, taifa na kufuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa chini ya wakufunzi kutoka klabu ya Manchester United ya Uingereza.
Aliongeza kuwa mwaka huu kutakuwa na mashindano ya siku nne ya timu bingwa kutoka kila nchi itakayoshiriki michuano hiyo, kushindania taji jipya la Airtel Rising Stars African Champion.

“Tumeamua kuongeza mshindano ya nchi na nchi mwaka huu, kwa nia ya kuweza kuwafanya vijana kushirikiana na kuwaleta karibu kwa kupitia njia ya pamoja, ambayo ni mchezo wa kandanda. Tunaamini ya kwamba michuano hii italeta hamasa na umoja kwa wachezaji,” alisema.
Kwa mwaka huu, michuano hii imezinduliwa na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Quinton Fortune, ambaye alisajiliwa na Sir Alex Ferguson mwaka 1999, akitokea Atletico Madrid, wakati huo akiimarisha timu yake kushinda mataji

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII