39 wahojiwa kuhusu mauaji SAUT
By Maganga Media - May 10, 2012
POLISI mkoani Mwanza inawashikilia watu 39 waliokamatwa katika msako uliofanyika maeneo ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine(Saut) kwa mahojiano juu ya mauaji ya utata yaliyotokea katika hosteli za wanafunzi wa chuo hicho. Mauaji hayo yalitokea kati ya Machi 9 hadi Mei 4, mwaka huu ambapo watu sita akiwemo mwanafunzi wa Saut waliuawa na watu wasiojulikana na wengine miili yao kuchomwa moto.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Deusdedit Nsimeki alisema msako huo ulianza mwishoni mwa wiki iliyopita na kwamba watuhumiwa hao wanafanyiwa mahojiano ili kuwabaini walioshiriki kwenye vitendo vya mauaji. Alisema uongozi wa Polisi umefanya mkutano na uongozi wa Saut juu ya kauli za wananchi zinazohatarisha amani ya wanachuo kutokana na mauaji hayo.
Alisema chuo kimeahidi kutoa ushirikiano na kwamba polisi itakutana pia na wamiliki wa hosteli za wanafunzi kuzungumza nao juu ya kuimarisha ulinzi kwenye hosteli hizo zenye wanafunzi 137, ikiwa ni pamoja na kuchanganya wanachuo wa jinsi tofauti.
Waliouawa katika kipindi hicho ni pamoja na Reginald Arbogast (24) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Saut, Mikidadi Mkiroba (29) na wengine wanne ambapo hawakufahamika majina yao wala mahali wanapoishi.
Katika tukio jingine, Ofisa Tabibu wa kituo cha afya cha Nange wilayani Misungwi, Evarist Nyangingili (51) amefariki dunia baada ya kupinduka na pikipiki Mei 4 mwaka huu katika Kijiji cha Nange kata ya Igokelo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII