HABARI MPYA LEO  

TAMASHA LA PASAKA - DODOMA

By Maganga Media - Apr 10, 2012

 Mwimbaji wa muziki wa injili Upendo Nkone akiwaimbisha washabiki wa muziki wa injili katika Tamasha la muziki la Pasaka linaloendelea jioni hii kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma kumefurika mashabiki wengi katika uwanja huo na watu wanafurahi kwelikweli kama wanavyoonekana wakinyanyua mikono yao juujuu.

Jana Tamasha hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku waimbaji wakubwa kutoka Nje ya Tanzania na ndani ya nchi wakifanya mambo makubwa kwa mwenyezi mungu 
 

 Mwimbaji Anastazia Mukabwa kutoka nchini Kenya akifanya mambo makubwa huku mashabiki wakifurahia burudani hiyo wakati akiwaambia wavue viatu.
 Mwimbaji Anastazia Mukabwa kutoka nchini Kenya naye akiimbisha mashabiki wake
 Kundi la Worriars Band likifanya vitu vyake jukwaani kama linavyoonekana katika picha.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama akifafanua jambo kwa MC wa Tamasha hilo MC Mwakipesile, katikati ni mratibu wa Tamasha Hudson Kamoga.
 

NAIBU SPIKA JOB NDUGAI AFURAHISHWA NA TAMASHA LA PASAKA DODOMA

 Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai akipokea CD kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, inayoitwa "Utukufu Kwa Mungu"ya muziki wa injiili kutoka kwa  Mwanamuziki Solomon Mukubwa wa DRC Congo,  iliyozinduliwa jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernald Membe

Tamasha lingine kubwa limefanyika leo kwenye uwanja wa Jamhuti mjini Dodoma likishirikisha waimbaji lukuki kutoka hapa nchini na nje ya nchi kufuatia lile la jana kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ambapo mwimbaji wa Afrika ya Kusini Rebecca Malope alitumuiza.
 Mkuu wa Mkoa  waa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi akipokea CD yake ya Utukufu kwa Mungu kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Betty Mkwasa akipokea CD yake ya Utukufu kwa Mungu kutoka kwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
 Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka Mkoani Dodoma Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza katika tamasha hilo leo jioni kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi na kushoto ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi na kushoto akiongea na wanadodoma kwenye tamasha hilo ambapo aliwahimiza wananchi wa Dodoma kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya amani nchini, Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Job Nduga na katikati ni Alex Msama. 
 
 
 

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII