SIMBA YAPETA KWA MBINDE
By Maganga Media - Apr 7, 2012
Timu ya soka ya Simba sc ya jijini Dar es Salaam imefanikiwa kusonga mbele kwa hatua nyingine ya michuano ya kombe la shirikisho. Ikiwa uwanjani katika mechi ya marudiano na timu ya Es Satif ya nchini humo jana usiku huko Aljeria, ilifanikiwa kusonge mbele licha ya kufungwa 3 kwa moja. Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa ni Es Satif 3 - 1 Simba SC.
Bao pekee la Simba lilifungwa na mchezaji wake Emmanuel Okwi dakika ya 91 na hivyo simba kufanikiwa kusonga mbele baada ya mechi ya awali iliyochezwa jijini Dar es Salaam kushinda 2 bila.
Katika mchezo huo, Simba ilipata pigo mapema dakika ya 18 baada ya beki wake Juma Said Nyosso kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza ‘rafu ya wazi’. Hadi mapumziko, tayari Setif walikuwa mbele kwa mabao 2-0 na mapema kipindi cha pili, wakapiga la tatu. Mchezo wa kwanza Simba ilishinda 2-0 Dar es Salaam.
Baada ya hatua hiyo sasa itamenyana na Al Ahly ya Sudan.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII