Romney apewa kipaumbele kuchuana na Obama
By Maganga Media - Apr 12, 2012
Mjumbe wa chama cha Republican Rick Santorum aliekuwa anawania nafasi ya kuteuliwa ili kugombea urais wa Marekani mnamo mwezi wa Novemba amejitoa kwenye kinyang'anyiro hicho. Rick Santorum aliyekuwa mshindani mkuu wa Mitt Romney ameamua kuisimamisha kampeni yake ya kuwania kuteuliwa na chama chake cha Republican ili kugombea Urais wa Marekani mnamo wa Novemba dhidi ya Rais Barack Obama.
Santorum aliwaambia waandishi wa habari mjini Gettysburg katika jimbo lake la uzawa la Pennyslvania kwamba kampeni ya kuwania uteuzi wa chama chake ili kugombea urais imefikia tamati kwake. ''Tulipitisha uamuzi wa kuingia katika kinyang'anyiro hiki tukiwa kwenye meza ya jikoni-katika muktadha wa vipingamizi vyote, na tuliamua mwishoni mwa wiki, kwamba wakati wa kinyang'anyiro hiki kwangu umefikia mwisho na kusimamisha kampeni, mapambano bado yanaendelea" Alisema Santorum.
| Miongoni mwa wagombea 4 wa chama cha Republican |
Hapo mwanzoni Satorum aliwashangaza watu baada ya kushinda katika hatua ya kwanza ya uteuzi wa chama chake katika jimbo la Iowa mnamo mwezi wa Januari. Santoruma pia alishinda katika majimbo mengine 10 lakini alishindwa kuishikilia pinduli ili kuweza kumpita mshindani wake mkuu Mitt Romney ambae sasa anaongoza katika kampeni ya kuwania kuteuliwa na chama chake ili asimame dhidi ya Rais Obama mnamo mwezi wa Novemba.
Santoram aliewahi kuwa Seneta wa jimbo la Pennyslavia amesema licha ya kujiweka kando ya kampeni , ameahidi kufanya kila atakaloliweza ili kukiunga mkono chama chake cha Republican ili kukishinda chama cha Rais Obama cha Demokratik.
Mitt Romney sasa ana nafasi kubwa ya kupambana na Rais Barack Obama katika uchaguzi wa Novemba.
| Mitt Romney |
Kamati ya kitaifa ya chama cha Republican imeusifu uamuzi wa Santorum wa kujiengua.
Mwanasiasa huyo ambaye ni muumini wa moyo wa kanisa katoliki anatetea sera za mrengo mkali wa kulia juu ya dini. Msimamo wake thabiti wa kupinga kutoa ujauzito na kupinga ndoa za mashoga uliitikiwa vizuri na wahafidhina. Lakini msimamo huo ulikuwa unawetenga wamarekani wenye siasa za ukadirifu.
Njia sasa ipo wazi kwa mshindani wake mkuu Mitt Romney ya kupata tikeki ya chama cha Republican ili kupambana na Obama katika uchaguzi wa rais mwezi wa Novemba. Lakini anahitaji kura 1144 za wajumbe ili kuweza kuipata tiketi hiyo kwenye mkutano mkuu utakaofanyika Tampa mwezi wa Agosti.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII