HABARI MPYA LEO  

Dk Bilal Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela

By Maganga Media - Apr 13, 2012

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemteua Dk. Mohamed Gharib Bilal kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, Aprili 11, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema Rais Kikwete pia amemteua Profesa David Homeli Mwakyusa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha chuo hicho cha Nelson Mandela.

Taarifa imesema kuwa uteuzi wa Dk. Bilal ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Profesa Mwakyusa aliyepata kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika Serikali ya Rais Kikwete ulianza Alhamisi iliyopita, Aprili 5, 2012.

Chuo cha Nelson Mandela ambacho kiko Arusha ni moja ya vyuo vikuu vinne vinavyolenga kuendeleza sayansi na teknolojia katika Bara la Afrika.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII