Arsenal yaizamisha Man City 1-0, Man U yajikita kileleni
By Maganga Media - Apr 8, 2012
Mkwaju wa mbali wa Mikel Arteta umeipa Arsenal ushindi muhimu na kuiacha Manchester City ikiwa pointi nane nyuma ya Manchester United katika ligi kuu ya England.
Mara mbili Robin Van Persie aligonga mwamba huku mkwaju mwingine aliopachika wavuni ukiwa wa kuotea. Arteta alipata mwanya katika dakika ya 86 kwa kuachia mkwaju umbali wa yadi 25.
Arsenal sasa wamerejea katika nafasi ya tatu, pointi mbili juu ya Tottenham walio nafasi ya nne.
Shuti kali la Scholes lilihakikisha ushindi wa United |
Man United sasa imefikisha pointi 79, City ikifuatia na pointi 71 ikiwa imesalia michezo sita kumalizika kwa ligi.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII