HABARI MPYA LEO  

Mancini ataka wachezaji wapimwe zaidi

By Maganga Media - Mar 21, 2012

Roberto Mancini

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amesema wachezaji wa Ligi Kuu hawana budi wapimwe afya zao mara mbili kwa mwaka.  Mancini anahisi utaratibu wa upimaji wa sasa "hauna uhakika" sana.
"Wakati nilipoangalia utaratibu wetu wa matibabu miaka miwili iliyopita, niliingiwa na hofu. Nilisema tunahitaji kufanya zaidi ya hapa," alisema.

Mancini ametoa maoni yake baada ya Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu Richard Scudamore kusema kutakuwa na utaratibu wa kupitia masuala ya upimaji baada ya Fabrice Muamba kuanguka na kuzirai kutokana na matatizo ya moyo

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII