HABARI MPYA LEO  

FIFA KUTOA BIMA KWA WACHEZAJI

By Maganga Media - Mar 22, 2012

Sepp Blatter rais wa shirikisho la soka duniani duniani FIFA

Rais was shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema shirikisho hilo litahakikisha kuwa wachezaji wote wanapata bima ya afya  wakati wanapocheza katika mechi zote za kimataifa. Blatter amewaambia wajumbe wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuwa,vyama vya soka kote duniani vitatia saini makubaliano hayo kufikia mwezi Mei mwaka huu.


Wachezaji watakaonufaika na mpango huo ni wale wote watakaochezea timu zao za taifa na vlabu katika mechi zote zinazotambuliwa na FIFA. Tayari shirikisho la soka barani Ulaya Uefa, limetangaza kuwa litaanza zoezi la kutoa bima kwa wachezaji wote wakati wa michuano ya bara Ulaya  baadaye mwaka huu.

Maganga Media

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII