Kifaa cha kujipima UKIMWI mwenyewe kipo sokoni!
By Unknown - Jul 4, 2012
Kwa mara ya kwanza kifaa cha kujipima iwapo mtu ana virusi vinavyosababisha ukimwi kimeidhinishwa na wataalam wanaodhibiti sekta ya Afya nchini Marekani. Kifaa hicho kwa jina OraQuick kitawezesha watu kutumia mate kuchunguza kama wana virusi vya ukimwi. Itachukua muda wa kati ya dakika 20 na 40 kubaini matokeo ya uchunguzi huo.
Kifaa hicho ambacho kitawezesha mtu kuchunguza hali yake mwenyewe nyumbani au kokote anakotaka kitaanza kuuzwa nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka huu. Serikali ya Marekani inatarajia kuwa kifaa hicho kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia miongoni mwa watu wanaoishi na virusi bila kujua.
Inakadiriwa kuwa robo millioni ya Wamarekani wako katika kitengo hicho. Utafiti wa kimatibabu unaoyesha kuwa majaribio ya matokeo ya uchunguzi wa kifaa hicho cha Oraquick yananaweza kuwa sahihi kwa asilimia tisini na mbili, miongoni mwa watu wanoishi na virusi vya ukimwi.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII