Uwoya nitasaidia kupatikana vazi la Taifa
By Unknown - Jun 24, 2012
ANAJULIKANA kwa kuvaa nguo zile zinazopigwa vita na wazazi na wadau mbalimbali, wengi wanasema zinakiuka maadili lakini cha kustaajabisha mtu huyu huyu anaibuka na kusema kuwa atasaidia kupatikana vazi la taifa.
Si mwingine ni Irene Uwoya staa aliyewahi kufanya vizuri katika filamu za Diversion of Love, Oprah, Off Side, Dj Benny na nyingine nyingi.
Kila mtu ana malengo yake, yeye amejikita kuhakikisha anatoa mchango kwenye vazi la taifa, je ni kwa namna gani atawezesha hili na je halitakuwa moja kati ya yale anayopendelea yeye? Huyu hapa anafunguka:
Mikakati yangu ya baadae kwanza kabisa ni kutengeneza filamu za kuitangaza nchi yangu, ambazo nitajitahidi kutumia mavazi ya kitamaduni ili kusaidia zoezi la kuwa na vazi la Taifa.
nimeamua hivyo kwa sababu naona wivu sana ninapoona wenzetu kwa mfano Wanaigeria ,Waghana na Waafrika ya Kusini katika filamu zao wanavaa mavazi yanayotambulisha asili za nyumbani kwao na sisi tunanunua na kuzipenda kwa nini na sisi tusiwe na vazi la Taifa letu,ambalo litatufanya tujivunie mbele za watu.
Mkakati wangi mwingine ni kujua vivutio vyetu,kiukweli hapa nilipo niambie nikuelezee kuhusu mlima KIlimanjaro nitatoa macho,na sio huo tu vivutio vyote nivijue hata nikiamshwa usingizini iwe rahisi kwangu kuvielezea na inawezekana kwa kuwa vipo ndani ya nchi yangu kwa nini nisivijue.
Penye nia pana njia lengo langu ni kwenda shule kabisa nikasomee masuala ya utalii kwanza kabla ya kufanya ziara katika hivyo vivutio, ili njionee kwa macho huwezi amini sijawahi kwenda kwenye mbuga ya wanyama ya hapa nchini hata moja na sasa ndio wakati wangu wa kufanya hivyo,na kuiweli sina mzaha na hilo. Kwa sababu miongoni mwa mambo ambayo napanga kufanya ni kuhakikisha nafanya filamu za kuitangaza nchi yangu na vivutio vyake.
Akizungumzia ziara yake aliyoifanya Kongo amesema alienda kwa ajili ya Tamasha la kumuenzi marehemu Steven Kanumba na waliitwa yeye na Patcho Mwamba. Amesisitiza kuwa anapata mialiko mingi sana kiasi kwamba hadi anaona kero. Hadi sasa anapokea barua pepe za kutaka afanye nao kazi lakini ana programu imenibana ikiwemo kusoma hayo mambo ya utalii lakini muda ukimruhusu, atafanya hivyo lengo ni kufanya kazi ambazo zitatambulika na nchi nyingi ikiwezekana Kimataifa. Furaha yake ni kuona mashabiki wanazifurahia kazi zake.
"Mafanikio ni mengi lakini kubwa ni kuanzisha Kampuni yangu iitwayo Sweet Afrika Entertainment,lakini kufanya muvi ambayo imepatia fedha nyingi iitwayo 'Mtihani'.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII