Ukraine yahalalisha biashara ya Ukahaba fainali za EURO
By Maganga Media - Jun 12, 2012
Ukraine imehalalisha masuala ya ukahaba kwamba si tena biashara haramu na kutoa nafasi kwa machangudoa kuzitumia Fainali za Euro 2012 kutengeneza 'noti' Pamoja na ruhusa hiyo, wanaharakati wa masuala ya jinsia wanapinga kuhalalishwa huko na kusema hadi kumalizika kwa fainali, sehemu kubwa ya mashabiki watakuwa wameambuikizwa HIV katika taifa hilo la Mashariki mwa Ulaya. Ukraine ilihalalisha biashara hiyo mwaka 2006, baada ya miaka ya nyuma kuwapiga faini za dola 6.5 hadi 16 na kati ya 10na 25 waliokamatwa kujihusisha na biashara hiyo haramu.
Inasadikiwa machangudoa kati ya 52,000 na 83,000 wako nchini humo na machangudoa zaidi ya 11,000 wako Kiev kwa ajili ya kusaka wateja kwa mujibu wa Taasisi ya International HIV/AIDS Alliance. Kwenye miji ya Donetsk na Kharkiv Mashariki, kuna machangudoa zaidi ya 3,000, na Lviv uliopo Kaskazini wanakadiriwa kufikia 2,500.
Kwa sasa miji hiyo imekusanya maelfu kwa maelfu ya mashabiki waliokuja kushuhudia Fainali za Euro 2012, zilizoanza Ijumaa iliyopita kwenye miji ya Warsaw, Poland, na fainali zake zitakuwa Kiev Julai 1. Wanawake wanaopinga biashara ya ukahaba, Femen ambao hupinga mambo kwa kuacha maziwa wazi, walisema wanapinga Fainali za Euro kwa kuwa zinachocheza biashara ya ukahaba na maambukizi ya HIV.
Akiwa anafanya mambo yake kwa siri katika viunga vya Kiev, msichana wa miaka 24, Natasha anasema anataraji kupata wateja wengi katika fainali hizi na atakapopata fedha atanunua gari, licha ya kulalamika kuwa wateja wengi 'wanawapotezea' na zaidi wanachenguka kwa soka na pombe. "Natarajia kupata fedha nyingi kwa sasa, tatizo lililopo ni kwamba wanaume wengi wanawehuka na mpira na kunywa sana pombe na wakikuchukua wanataka mkanywe tu nami nataka pesa," aliiambia AFP katika mahojiano.
Kutokana na kufurika kwa mashabiki ambao wengi ni wenye fedha zao kutoka Mataifa ya Ulaya Magharibi, machangudoa wengi wamepandisha dau," anasema Olena Tsukerman mmoja wa wamiliki wa madanguro. "Mbali na hao, pia kuna machangudoa wanaoitwa 'VIP', hawa ni wale wanaofahamu lugha za mataifa mbalimbali ambao huchaji wateja kwa kati ya Euro 100 (Tsh 200,000) na 200 (Tsh400,000) kwa saa, na wanaweza kuongeza hadi mara tatu yake," Tsukerman anasema.
"Fainali zimeanza na tayari kila mmoja (changudoa) amekwishapandisha dau. Lakini ili kuvutia biashara wameambizana isiumize sana kwani wanaweza kukosa wateja," alisema huku akilalamika kuwa walikwenda Ujerumani kwenye Fainali za Kombe la Dunia 2006 na walipata hasara.
Msemaji wa Taasisi ya International HIV/AIDS Alliance, Kostyantyn Pertsovski anasema: "Hakuna mahala panapoonyesha watakaoingia Ukraine ni walevi wa ngono. Mashabiki wengi zaidi wanazama kwenye ulevi wa pombe." Tsukerman anasema pia kuwa polisi wamekuwa wakihongwa na machangudoa ili kuwaachia waendelee na biashara yao katika maeneo ambayo hawaruhusiwi kuonekana.
Mashabiki wanaofanya ngono wako katika hatari kubwa: Ukraine ambayo iliyo Ulaya Mashariki ikipakana na Asia ya Kati ni moja ya mataifa yenye viwango vikubwa vya maambukizi ya HIV na sehemu kubwa ni ngono zembe zinazosababishwa na pombe.
Kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS, watu 350,000 wenye umri kati ya miaka 15 na kuendelea kwa taifa hilo lenye watu 46 milioni wanaishi na virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi.

Yulia ni mmoja lakini wako wengi kwenye mji wa Kiev. Anatoka Kaskazini mwa Ukraine ambako wanaishi watu mafukara. Wazazi wake wote hawana kazi na Yulia hajaenda shule, hana kazi wala hakuna familia ya kuwapa msaada na ndicho kilichomfanya kuanza ukahaba akiwa na miaka 18.
Kwa sasa anapata dola 1,250 kwa mwezi na anapata wateja kati ya wawili hadi watatu kwa siku kwenye hoteli, hosteli za wageni na barabarani. Fedha anazopata ni nyingi japo zina madhila yake kwani watu wengi hupata dola375 kwa mwezi.
"Kimwili, kiroho na kisaikolojia ni ngumu. Kila mteja anataka kufanywa anavyotaka," Yulia anasema huku akitaka machangudoa wenzake wa Kiev kupimwa HIV na pia anasisitiza matumizi ya kondom.
"Si rahisi, tunaogopa sana. Kila mtu anahofia kuona kile asichoona, Kitakachotokea na anachotarajia. Lolote linaweza kutokea." Unapoitwa, unakwenda na unakutana na mteja mmoja lakini wakati mwingine wanakuwa wawili na kumbaka. "Sikuweza kutoka kwenye hosteli, sikuwa na la kufanya nilichofanya ni kuwaachia, nikafumba macho wakafanya walivyotaka."

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII