HABARI MPYA LEO  

Uhispania yatinga nusu fainali

By Emmanuel Maganga - Jun 24, 2012

Xabi Alonso

Alonso aliifungia Uhispania bao la kwanza dakika ya 20 na la pili la penalti dakika ya 91

Mabingwa watetezi wa Euro 2012 waliweza kuishinda Ufaransa magoli 2-0, timu ambayo wakati mwingine ilionyesha ustadi wao katika mchezo, lakini kwa jumla wakiwa dhaifu na kukosa mbinu walipolifikia lango la wapinzani wao.

Uhispania, baada ya ushindi huo katika uwanja wa Donetsk usiku wa Jumamosi, sasa itakutana na Ureno katika mechi ya nusu fainali. Jordi Alba, kwa haraka haraka alifanikiwa kumchenga mlinzi aliyemuandama na kuupiga mpira juujuu, na ambao ulimfikia Xabi Alonso, ambaye pasipo kusita alikuwa ameusubiri kwa makini, na kuusindikiza kwa kichwa hadi wavuni, akiandikisha bao la Uhispania baada ya dakika ya 20 za mchezo.

Kwa kawaida Xabi Alonso huwa hakosi kufunga mikwaju ya penalti inapojitokeza, na katika dakika ya 91, aliweza kufunga bao la pili, na akiuelekeza mpira hadi kona ya lango.

Kwa mbinu hafifu Ufaransa ilijitahidi kuitisha Uhispania, lakini juhudi zao za pekee zilizokaribia kuandikisha bao ni wakati Mathieu Debuchy alipousindikiza mpira kwa kichwa kuelekea wavuni baada ya kupigiwa mpira na Franck Ribery.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII