Nahodha wa zamani Ireland afariki
By Unknown - Jun 24, 2012
Kocha wa zamani wa timu ya soka ya Ireland ya Kaskazini, Alan McDonald, amefariki ghafula akiwa na umri wa miaka 48. Alizimia na kufariki ghafula akicheza golf
McDonald, ambaye alikuwa ni meneja wa timu ya Glentoran wakati ilipochukua ubingwa wa ligi ya Ireland mwaka 2009, alizimia alipokuwa akicheza golf Jumamosi asubuhi.
McDonald, aliyekuwa mchezaji wa kati katika soka, alizaliwa mjini Belfast, na alikuwemo katika timu ya Ireland ya Kaskazini ambayo ilitoka 0-0 dhidi ya England katika mechi ya mwaka 1985, na kuiwezesha nchi yake kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia. Aliichezea timu ya Ireland ya Kaskazini mechi 52.
Alifanikiwa kuifungia timu bao moja, wakati walipocheza dhidi ya Denmark mwaka 1986.
Habari za kifo chake ni pigo kubwa kwa wapenda soka katika Ireland ya Kaskazini. Alikuwa na biashara ya kuuza tuzo mbalimbali za michezo mjini Bangor, biashara ambayo awali ilikuwa ikiendeshwa na mchezaji mwenzake katika timu ya taifa, Billy Hamilton.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII