Marekani yahofia kutokea ugaidi Kenya
By Unknown - Jun 24, 2012
Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umeonya kwamba kuna tishio la shambulio la kigaidi kutokea mjini Mombasa karibuni, na umewataka watumishi wa serikali ya Marekani kuondoka katika mji huo.
Hii siyo mara ya kwanza kwa onyo kama hilo kutolewa. Mwezi wa Oktoba mwaka jana, ubalozi wa Marekani ulisema kuna tishio la shambulio kwenye maeneo ambayo hutembelewa na wageni kama vile maeneo ya maduka mengi na vilabu vya starehe. Wakati huo hakuna lilotokea, lakini hali katika nchi ya jirani, yaani Somalia, imezidisha wasiwasi.
Marekani imehusika na mapambano dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, ambao baadhi yao wana maingiliano na jamii kubwa ya Wasomali inayoishi Kenya. Marekani haitaki kupita tena kwenye maafa ya mwaka wa 1998, ambapo ubalozi wake mjini Nairobi ulishambuliwa kwa mabomu, na watu zaidi ya 200 walikufa.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII