HABARI MPYA LEO  

Tanzania Na China Za Jivunia Mafanikio Ya Matumizi Ya Teknolojia Katika Kilimo

By Unknown - Jun 25, 2012



Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini Tanzania kuhusu mikakati ya serikali ya kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania.






Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini.



Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza hafla fupi ya kusherehekea mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania Bw.

Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.





Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa reli ya Uhuru (TAZARA) walioalikwa kwenye hafla hiyo Bw. Abdul Haji (kulia) na mama Roza Kangoma (kulia) ambaye ni mama wa balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha mafunzo cha TAZARA.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII