Okwi, Kaseja watajwa kuwania tuzo
By Maganga Media - Jun 10, 2012
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Uganda na timu ya Simba, Emmanuel Okwi, watachuana na kiungo wa Kimataifa wa timu ya Taifa ya Rwanda na Yanga Haruna Niyonzima kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka kwa wachezaji wa kigeni nchini inayosimamiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa). Mwingine wa kigeni alioingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni na Kipre Tchetche wa Ivory Coast anayechezea Azam FC.
Akizungumza katika hafla fupi ya kutaja majina ya wachezaji wa ndani na nje watakaowania tuzo hizo, Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hizo Masoud Sanan alisema kwa upande wa wanasoka wazalendo, wanaowania ni John Bocco, Aggrey Morris wote wa Azam na Juma Kaseja wa Simba.
Kwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza soka nje ya nchi ni Henry Joseph wa Kongsvinger ya Norway na Mbwana Samatta wa Tout Puissant Mazembe ya DRC.
Sanan alisema kwa wanawake wanaowania tuzo hizo ni pamoja na Sophia Mwasikili anayecheza Uturuki, anashindana na Asha Rashid ‘Mwalala’, Mwanahamisi Omary wote wa Mburahati Queens, Fatuma Mustapha wa Sayari na Eto’o Mlenzi wa JKT. "Siku hiyo atatangazwa mshindi wa tuzo ya heshima kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo mshindi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tatu, Benjamini Mkapa," alisema Sanan.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII