HABARI MPYA LEO  

Mazungumzo yaendelea Sudan

By Unknown - Jun 25, 2012

Mazungumzo yanaendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia, kujaribu kumaliza mzozo wa mpaka baina ya Sudan na Sudan Kusini, ambao katika miezi ya karibuni ulitishia kuzusha vita kamili.

Thabo Mbeki anaongoza mazungumzo ya amani ya Sudan

Tatizo kuu ni wapi kuweka mstari wa mpaka utakaotenganisha nchi mbili hizo, na kuweka eneo la amani la mpakani. Ingawa wapatanishi wamezihakikishia pande zote mbili, kwamba mstari huo utakuwa wa muda tu, hata hivo Sudan na Sudan Kusini hawaamini hayo - wanaona mwishowe utakuwa mpaka wa kudumu baina yao.

Mazungumzo ya upatanishi yanaongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, na yanaungwa mkono na nchi jirani, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII