HABARI MPYA LEO  

Maafisa wa ICC watupwa jela Libya kwa kuvujisha nyaraka za kesi ya mtoto wa Gaddafi

By Maganga Media - Jun 12, 2012


Ajami al-Ateri kiongozi wa kundi la wapiganaji la Zintan brigade, linalomzuilia Saif al-Islam Gaddafi
Maafisa wanne wa mahakama ya ICC nchini Libya wamewekwa jela. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa kundi moja la wapiganaji nchini Libya. Inaarifiwa wanne hao walizuiliwa mnamo Alhamisi na wataendelea kufungwa kwa siku 45 wakisubiri uchunguzi.

Mmoja wa maafisa hao , wakili Melinda Taylor, anatuhumiwa kwa kujaribu kumkabidhi stakabadhi mwanawe hayati Muamar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi anayezuiliwa na kundi la wapiganaji la Zintan brigade ambalo limekuwa likimzuilia tangu mwezi Novemba. Wanne hao walihamishwa hadi jela kwa amri ya mwanasheria mkuu na maafisa wa wizara ya ulinzi, kulingana na Ajami al-Ateri kiongozi wa kundi hilo la Zintan brigade.
Ateri alisema kuwa maandamano yatafanyika kutaka wanne hao kufunguliwa mashtaka.

Taarifa za wizara ya mambo ya nje ya Libya zilithibitisha wanne hao kuzuiliwa kwa siku 45 ingawa alikanusha kuwa wako jela.Maafisa wa utawala nchini Australia wamesema wanatafuta njia za kidiplomasia kuweza kumfikia mmoja wa wajumbe hao Bi Taylor ambaye ni raia wa nchi hiyo pamoja na maelezo kuhusu sababu zililosababisha kuzuiliwa kwake. Ujumbe mwingine wa ICC uliwasili nchini Libya mnamo Jumapili, katika juhudi za kutaka maafisa hao kuachiliwa.
Saif al Islam

Wanachama wa kundi hilo la Zintan wanadai kuwa wajumbe hao walikuwa wamebeba nyaraka ikiwemo barua kutoka kwa rafiki wa karibu wa Saif A Islam ambaye yuko nchini Misri. Inaarifiwa barua hiyo ilikuwa na picha pamoja na alama ambazo zilieleweka tu kwa mwenye kuutuma ujumbe huo pamoja na Saif al-Islam mwenyewe, alisema balozi wa Libya katika mahakama ya ICC.

Saif al-Islam, alikamatwa Novemba mwaka jana na kundi hilo la wapiganaji wakati akijaribu kutoroka. Anatakikana na ICC kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu. Ingawa serikali ya muda ya Libya imekataa kumkabidhi kwa ICC iksema ni bora mahakama ya Libya iweze kusikiliza kesi dhidi yake.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII