HABARI MPYA LEO  

JK awaapisha mabalozi 10

By Maganga Media - Jun 12, 2012

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jana amewaapisha mabalozi wapya kumi ambao wataongoza idara na kurugenzi mbalimbali katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani Rais akimuapisha Balozi Bertha Semu Somi ikulu Jijini Dar es Salaam leo.
Balozi Celestine Joseph Mushy akila kiapo.


MABALOZI wapya walioapishwa jana wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.Naimi Asizi (Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda), Dora Msechu (Mkrugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika), Ramadhan Mwinyi (Naibu balozi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa)  na Irene Kasyanja (Mkurugenzi kitengo cha Sheria).


Wengine ni Vicent Kibwana (Mkurugenzi Idara ya Afrika), Celestin Mushy (Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa), Hassan Yahya (Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati), Silima Kombo Haji (Mkurugenzi wa Mambo ya nje Zanzibar) na Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi wa Asia na Australia).

Pichani Rais akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.Kutoka kushoto walisimama mstari wa mbele ni Balozi Bertha Semu Somi,Balozi Hassan Simba Yahya, Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana,Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz,Balozi Irene Mkwawa Kasyanju na Balozi Dora Mmari Msechu.Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji,Balozi Celestine Joseph Mushy, Balozi Mbelwa Brighton Kairuki na Balozi Ramadhan Muombwa Haji


Akizungumza baada ya hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema hadi sasa kuna mabaliozi 32 walioko nje ya nchi na kwamba sasa wamefikia 42 na kwamba wamezingatia jinsia, umri na muungano katika kuteua mabalozi hao.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII