HABARI MPYA LEO  

BBA: Goldie amwokoa Prezzo

By Emmanuel Maganga - Jun 20, 2012


Wiki hii kwenye shindano la Big Brother Africa, Goldie alishinda zoezi la mwanzo wa wiki na kumfanya awe mkuu wa nyumba (HoH) kwa wiki moja. Hiyo ina maana kuwa unapokuja muda wa nomination , atakuwa na nafasi ya kumwokoa mtu mmoja na kumbadilisha na mwingine.

Bahati mbaya ni kuwa washiriki wengine wa shindano hilo wameanza kumwekea mtimanyongo mfalme wa viwalo wa Kenya, Prezzo kwa kumtaja zaidi atoke wiki hii. Asilimia 41 za kura zote zilimwangukia yeye na hivyo kuhatarisha ukaaji wake kwenye mjengo huo wa BBA.

Biggie aliposoma majina ya wale watakaokuwa hatarini kutoka, Goldie alishangaa na kuvuta pumzi na kuitoa nje kwa mshtuko baada ya kusikia jina la mpenzi wake Prezzo limo. “Oh my God,” alisikika akisema.

Licha ya huzuni iliyojidhihirisha kwenye sauti yake, muda ulipofika wa kumtaja atakayemwokoa, hakufikiria mara mbili zaidi ya kumtaja Prezzo.

Reaction yake baada ya kusikia jina la Prezzo kuwa limo kwenye orodha ya watakaokabiliwa na eviction week hii na kitendo cha kumwokoa, kinaashiria kuwa kweli mrembo huyu wa Nigeria amekufa na kuoza kwa mnyamwezi Prezzo.

Huu ni wakati sasa wa Prezzo kuacha kumchukulia poa kama alivyofanya wiki kadhaa zilizopita kiasi cha kumfanya Goldie akatae kula na kuhofiwa huenda akataka kujuia.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII