Uchaguzi wa Misri kwenda raundi ya pili
By Maganga Media - May 26, 2012
Mgombea wa urais kutoka mrengo wa Muslim Brotherhood Mohammed Mursi anatarajiwa kuchuana na Waziri Mkuu wa zamani Ahmed Shafiq katika raundi ya pili kutokana na matokeo ya kura hadi sasa. Huku vituo 11,000 kati ya 13,000 zikiwa zimetangaza matokeo yake, Bw Mursi ameongoza kwa asili mia 26 ya kura naye Bw Shafiq amepata asili mia 24. Hamdin Sabbahi mbaye mkosoaji mkubwa wa uliokuwa utawala wa Mubarak anashikilia nafasi ya tatu.
Bw Musri anawakilisha mrengo mashuhuri ambao ulitengwa katika ulingo wa kisiasa kwa miaka mingi chini ya utawala wa Hosni Mubarak.Wagombea wawili wa kwanza wanawakilisha makundi mawili nchini Misri. Shafiq anatajwa na wakosoaji wa Mubarak kama kibaraka wa utawala ulioondolewa madarakani. Wadadisi wamesema ameungwa mkono na kundi la watu wanaohofia utawala wa vyama vinavyoegemea sera za kidini na wale ambao wanapinga msukosuko ambao umekuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Raundi ya pili ya uchaguzi wa urais ni mwezi Juni. Asili mia 50 ya wapiga kura wameshiriki uchaguzi wa sasa wa urais nchini Misri.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII