Mwanafunzi ajifungulia choo cha shule na kutupa kichanga!
By Maganga Media - May 26, 2012
JESHI la Polisi Mkoa wa Kigoma linamtafuta mwanafunzi wa kidato cha nne Rehema Issa (22) wa sekondari ya Rwiche kwa tuhuma za kutupa mtoto mchanga kwenye choo cha shule muda mfupi baada ya kujifungua. Kaimu Kamanda wa Mkoa huo Fransis Mwakabana alisema mwanafunzi huyo alifanya tukio hilo juzi saa saba mchana katika kijiji cha Kamara, kata ya Mngonya.
Kamanda Mwakabana alisema mwanafunzi huyo katika kipindi chote cha ujauzito wake walimu na wazazi wake hawakumgundua kwa sababu alikuwa anahudhuria masomo yake kama kawaida. Siku ya tukio mwanafunzi huyo alikwenda shule lakini baada ya muda uchungu ulimshika na kwenda chooni ambako alijifungua mtoto wa kiume na kumtupa kwenye shimo la choo cha shule hiyo.Wanafunzi waliokuwa wanataka kuingia chooni walisikia sauti ikitoka ndani ya shimo la choo na kuamua kumuokoa akiwa hai lakini baada ya muda mfupi alifariki.
Baada ya mwanafunzi kufanya mauaji hayo alitorokea kusikojulikana huku juhudi za kumtafuta zikiendelea, mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa kwenye hospital ya mkoa wa Kigoma kwa uchunguzi zaidi.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII