Tume Ya Katiba yapewa ofisi na vifaa
By Maganga Media - May 3, 2012
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Mwenyekiti Jaji Warioba (mbele katikati) pamoja na wadau wengine baada ya Tume kukabidhiwa Ofisi, Mtaa wa Ohio, Dar es Salaam leo. Kulia kwa Jaji Warioba ni Waziri Kombani na kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria ZNZ Abubakari Khamis Bakari. Wengine ni Makatibu Wakuu Viongozi Balozi O. Sefue (SJMT) na Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee (SMZ).

Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimtembeza Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba katika ofisi mpya ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo kwenye Wizara ya mambo ya ndani jijini Dar es salaam, katikati ni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba.

Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue kushoto akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya Waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba wakati wa makabidhiano ya ofisi ya Tume hiyo iliyopo katika jengo jipya la Wizara ya mambo ya Ndani ghorofa ya kwanza , wa pili kutoka kushotoni Celina Kombani Waziri wa Sheria na Katiba na Angela Kairuki mbunge wa CCM viti maalum Dar es salaam


Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba mpya wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya ofisi watakayoitumia.

Baadhi ya wajumbe wa Tume ya Kuratibu maoni ya Katiba mpya wakiingia kwenye ukumbi wa mikutano tayari kwa kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya ofisi watakayoitumia.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII