Mkutano kujadili uchumi wa Afrika
By Maganga Media - May 10, 2012
Mkutano wa viongozi wa kisiasa na wafanyabiashara wa Kimataifa wameanza mkutano mjini Addis Ababa,Ethiopia kujadili jinsi ya kukuza maendeleo na kuvutia uwekezaji katika bara hilo. Mkutano huo wa siku tatu juu ya Uchumi Duniani utaangazia masuala kama ajira, utawala bora na kutunza mazingira.
Watayarishi wa mkutano huu wanasema kua Afrika, ni bara lenye nchi sita zenye Uchumi unaokua kwa kasi Duniani na sasa bara hilo liko kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa ya uchumi.
Nigeria ni mojapo ya nchi hizo zenye Uchumi unaokua kwa kasi, lakini kama anavyoarifu mwandishi wa BBC Chris Ewokor kutoka Abuja, siyo kila mwananchi aliyenufaika na wimbi hili la mapato. Ewokor anasema kua majuma matatu yaliyopita Waziri mdogo wa Nigeria katika Wizara ya fedha, Dr Yerima Ngama,alitangaza kua nchi hiyo ni ya tatu kwa nchi zenye Uchumi unaokua kwa haraka.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII