Mke wa Sajuki aeleza hali ya Sajuki!
By Maganga Media - May 21, 2012
Mke wa Sajuki (Wastara) ambae yuko India kwa sasa akiwa anamuuguza mumewe (Sajuki) amezungumza kuhusu hali ya sasa ya Sajuki. Amesema kuwa Sajuki alikua hawezi hata kuongea ukamuelewa, sasa hivi anaongea hata kwa mda wa saa moja kitu ambacho alikua hawezi kabisa na sasa hivi ameweza kukaa kabisa”
Amesema “kwa kweli hali imebadilika na ninategemea kuona hali nzuri zaidi leo (Jumapili) ni siku ya tano toka tumekuja huku India, Sajuki amebadilika sana kwa sababu siku tulipoondoka Tanzania hali yake ilikua mbaya hata rangi alibadilika lakini kwa sasa amerudi kwenye hali ya kawaida”
Wastara. |
Wastara amesema changamoto inayowakabili ni namna ya kuwasiliana na madaktari na watu wengine wanaowahudumia kwani watu hao hawajui Kiingereza, sasa unaweza kukuta unahitaji kitu lakini hamuelewani. Kitu kingine ni swala la chakula, chakula ni kipya kwetu wote wawili huku ni Asia wana vyakula vyao”
Kuhusu Ugonjwa wa Sajuki, Wastara amesema walivyoondoka Tanzania walijua wanakwenda India na Sajuki atatibiwa ugonjwa unaomsumbua moja kwa moja lakini kabla ya kufanyiwa chochote ikagundulika kwamba alikua na tatizo la pumzi hivyo haikuwezekana kutibiwa ugonjwa wake kwa sababu inatakiwa kabla ya kufanyiwa opareshen anatakiwa kuwa kwenye hali ya kawaida, kwa hiyo ametibiwa kwanza tatizo la pumzi ili aweze kuhema vizuri ndio aanze kutibiwa ugonjwa wake”
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII