HABARI MPYA LEO  

Kesi ya Lulu; Upelelezi haujakaamilika

By Maganga Media - May 22, 2012

Imeripotiwa kuwa Upelelezi wa kesi ya muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na  kesi ya mauaji bado haujakamilika.Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Jana Wakili wa Serikali, Ladislaus Komanya aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba mahakama ipange tarehe nyingine.Hakimu Agustina Mmbando aliahirisha kesi hiyo na hadi June 4, 2012 itakapotajwa tena mahakamani hapo. Hata hivyo jana Mahakama ya Kisutu ilibidi itumie jalada la muda kwa kuwa jalada halisi la kesi hiyo limepelekwa Mahakama Kuu na hakimu Mmbando alisema kuwa bado halijarudi.

Jalada hilo lilipelekwa Mahakama Kuu Ijumaa ya Mei 18 baada ya jopo la Mawakili wa mshtakiwa  huyo kuwasilisha maombi huko juu ya uchunguzi kuhusiana na umri halali wa msanii huyo. Umri wa mshtakiwa huyo umezua utata kama ni mtoto au ni mtu mzima, jambo ambalo limewalazimu mawakili hao kuwasilisha maombi hayo ya uchunguzi wa umri wake Mahakama Kuu.

Maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo  na Wakili Peter Kibatala Mei 15, 2012 na yamepangwa kusikilizwa  na Jaji Dk Fauz Twaib Mei 28, 2012.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII