JB awavaa Africa Magic Swahili!
By Maganga Media - May 27, 2012
MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu Jacob Steven 'JB' amelalamikia malipo kidogo wanayolipwa na Mult Choice pindi wanapopeleka kazi zao ili zionekane kwenye stesheni ya Afrika Magic Swahili. Alisema malipo ndio sababu inayofanya hata kazi zinazoonekana huko hazina ubora unaotakiwa matokeo yake zinaonekana kazi za kawaida wakati Tanzania kwa sasa ipo juu kwenye masuala ya filamu.
JB alifafanua kuwa hafikirii kupeleka kazi yake huko kwani siku wanafungua stesheni hiyo alikuwepo na anajua wanacholipa hivyo kwa kazi za Kibongo zilivyo na gharama kuziandaa, inakuwa ngumu kuzitoa kwa malipo kiduchu.
"Kwanza kabisa lengo la kuanzishwa kwa stesheni ile ilikuwa ni kukikuza Kiswahili matokeo yake inaonekana kwenye nchi za Afika Mashariki ambazo baadhi yake wanakijua Kiswahili hivyo ili iwe na maana iende mbali ivuke ndio lengo la kukitangaza kiswahili litataimia"alisema na kuongeza kuwa , "Kwa malipo wanayolipa si rahisi kupata kitu ambacho wamekusudia ili waweze kuzitangaza filamu za Tanzania ni bora wakaongeza mapato lakini kwa ilivyo sasa ni sawa na kutoa bure ingawa ni mkataba na makubnaliano maalum lakini bado ni kidogo sana"alisema JB bila kuweka wazi ni shilingi ngapi.
Akijibu tuhuma hizo Ofisa Uhusiano wa MultChoice Barbara Kambogi, alisema kuwa hayo malalamiko tayari yanafanyiwa kazi hasa la malipo. "Malalamiko hayo yapo na yanafanyiwa kazi hasa ya malipo ingawa sio madogo kiasi hicho na kuhusiana na stesheni hiyo kuishia nchi za Afrika Mashariki linashughulikiwa na tatizo ni masafa na juhudi zinafanyika ili yapatikane marefu lakini vile vile hii chaneli ni changa ndio kwanza inaanza kujitanua kila pembe ya Dunia,"alisema Barbara.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII