HABARI MPYA LEO  

Wagombea walioshindwa wapinga matokeo Misri

By Maganga Media - May 28, 2012

Wagombea urais wawili walioshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi nchini Misri wametaka baadhi ya kura zihesabiwe tena, wakidai kulitokea udanganyifu.
Amr Moussa ataka mkuu wa mashtaka afanye uchunguzi
Afisa mmoja wa polisi aliwashutumu baadhi ya wenzake, kwamba waligawa kadi 900,000 za utambulishi, bila ya kutaja kazi yao, ili wapate kupiga kura.Wanajeshi hawaruhusiwi kupiga kura Misri.Msemaji wa Hamdeen Sabahi, kiongozi wa mrengo wa kushoto aliyetokea watatu, alisema kuwa watakata rufaa Jumapili, ili kuzuwia duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Waziri wa zamani wa mashauri ya nchi za nje, Amr Moussa, aliyemaliza wa tano, alimsihi afisa wa mashtaka kufanya uchunguzi. Kwa matokeo ya hadi sasa, duru ya pili ya uchaguzi itakuwa kati ya Ahmed Shafiq, waziri mkuu wa mwisho wa Hosni Mubarak, na Mohamed Mursi wa chama cha Muslim Brotherhood.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII