HABARI MPYA LEO  

Mbowe apata wakati mgumu kumlinda Shibuda!

By Maganga Media - May 27, 2012


 Wananchi wakitembea kwa mtindo wa maandamano kutoka eneo la mkutano jangwani kuelekea ofisi za CHADEMA kinondoni.
 Mh.Mbowe na Mnyika wakiwa wamesimama kwenye gari wakati wa matembezi wakitoka kwenye mkutano

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mh Freeman Mbowe jana alipata wakati mgumu wa kutuliza sauti za wananchi waliohudhuria mkutano wakimtaka kumtimua Shibuda kwa madai kuwa amekiuka taratibu za chama. Wakati akiendelea kusema hayo, umati uliokuwepo uwanjani hapo ulipokea kauli hiyo kwa kupaza sauti kwamba  “Shibuda ang’olewe …Shibuda ang’olewe… Shibuda aondoke!’ hoja iliyojibiwa na Mbowe papo kwa hapo  kwamba  mkutano huo haukuwa na lengo la kumng’oa mtu.

“Sikuja hapa kumng’oa mtu…Tumng’oe?” Alihoji Mbowe  na kuongeza: “Ngoja nitoe kauli ya chama.  Chama chetu hakitayumbishwa na mtu yeyote msaliti. Tutatumia vikao vya chama. Tuzungumze mambo yenye maslahi ya taifa, siyo mtu mmoja mwepesi. Kama mtu hajui moto auchezee.”  Alisisitiza kuwa chama hicho kimejengwa kwa zaidi ya miaka 20 na  kimeweza kujenga ngome katika mikoa ya Mwanza, Lindi na Mtwara.   

Huku akinukuu kauli ya Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliyoitoia miaka ya 1960, Mbowe alilitaka Jeshi la Polisi kutowatisha wanachama wa Chadema na kuonya kuwa wakifanya hivyo, wananchi nao watajibu mapigo.   “Chadema kitakuwa chama cha mwisho kuvuruga amani nchini. Nawaonya kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na kama Mwenyekiti wa Chadema na kama Mbunge. Nawaomba polisi, waache kuwasumbua wana Chadema,” alionya  Mbowe.   

Licha ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano ya wanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani, watu walianza kufurika katika Viwanja vya Jangwani kuanzia saa 8:00 mchana.  Kampeni ya Movement for Change(M4C)  Akizungumzia mkakati huo, aliwataka wanachama wa Chadema na wananchi kwa ujumla kujitolea kukichangia fedha ili kufanikisha kampeni hiyo kwani alisema kukiondoa CCM madarakani si kazi rahisi, inahitaji  gharama kubwa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII