HABARI MPYA LEO  

WAGOMBEA BUNGE LA EAC

By Maganga Media - Apr 15, 2012

WAGOMBEA 33 ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka vyama mbalimbali wamewekwa hadharani jana huku mchakato unaotumika sasa kuwapata wabunge hao ukipingwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Wagombea hao wanatoka katika vyama vya CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, TLP, UDP
na Tadea ambao taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya Bunge ilisema wagombea hao tayari wamerudisha fomu za kuomba nafasi hiyo ambapo uchaguzi wake unatarajiwa kufanyika keshokutwa.

Hata hivyo, mgombea mmoja hakutimiza masharti ya uchaguzi ya kuthibitisha uraia wake na
kulipa ada ya uchaguzi kwa mujibu wa kanuni ya Bunge, hali iliyofanya asiteuliwe.

Walioteuliwa kutembea nafasi hizo kundi la wanawake ni Angela Kizigha, Fancy Nkuhi, Dk. 
Godbertha Kinyondo, Janet Mmari, Janet Mbene, Maryam Ussi Yahya, Rose Mwalusamba, Shy-rose Bhanji, Sofia Rijaal na Septuu Nassor wote kutoka CCM.

Wagombea wa Zanzibar ni Abdullah Mwinyi, Ahmada Hamad Khatib, Dk. Haji Mwita Haji,
Khamis Jabir Makame, Dk. Said Gharib Bilal na Zubeir Ali Maulid. Wote hao ni kutoka CCM.

Wagombea kutoka vyama vya upinzani ni Anthony Komu (Chadema), Dk. Fortunatus Masha (UDP), Juju Danda (NCCR Mageuzi), Michael Mrindoko (TLP), Mwaiseje Polisya (NCCR Mageuzi), Nderakindo Kessy (NCCR Mageuzi) na Twaha Taslima (CUF).


Hata hivyo, Mrindoko amewekewa pingamizi baada ya wanachama watatu, Hamad Rajab
Tao, Othman Mgaza na James Haule kufungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania wakidai kulikuwa na ukiukwaji wa Katiba na kanuni za TLP katika uteuzi.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII