Simba na Yanga uwanjani kusaka pointi
By Maganga Media - Apr 15, 2012
MIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga leo itakuwa kwenye viwanja viwili tofauti ikisaka pointi tatu muhimu.
Vinara wa ligi hiyo, Simba watakuwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shooting.
Mechi hiyo ni muhimu kwa Simba kuibuka na ushindi ili iendelee kuongoza baada ya Azam jana kufikisha pointi 50 kwa kuifunga Polisi Dodoma bao 1-0.
Simba inaingia uwanjani kwenye Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya kutoka Algeria ilipokwenda kuiondoa ES Setif ya huko katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kwa upande wa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga, watakuwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kumenyana na wenyeji wao, Toto Africans.
Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 43 baada ya kupokwa pointi tatu ilizopata katika mechi dhidi ya Coastal Union kwa madai ya kumchezesha Nadir Haroub 'Canavaro' akiwa anatumikia adhabu.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII