Kesi ya Liyumba, Shahidi ahusishwa
By Maganga Media - Apr 15, 2012
UPANDE wa utetezi katika kesi kukutwa na simu gerezani akiwa mfungwa inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba umedai kuwa shahidi wa pili wa upande wa mashitaka naye anahusika katika kesi hiyo.
Akimhoji shahidi huyo anayeitwa Patrick, wakili Majura Magafu alidai kuwa shahidi huyo alikuwa akiitwa polisi zaidi ya mara moja kuandika maelezo ya nyongeza kwa sababu na yeye alikuwa ni mtuhumiwa katika kesi hiyo.
“Ulikuwa unaitwa kwa sababu na wewe ulikuwa ni mtuhumiwa katika kesi hii ulikuwa unashukiwa kuwa ni wewe uliyeingiza simu hiyo gerezani kama kweli ilikamatwa huko,” alidai Magafu ambapo shahidi alikataa kuwa si kweli.
Awali Magafu alitaka ufafanuzi ni kwanini tukio lilitokea Julai 27, 2011 lakini maelezo ya shahidi huyo yalitolewa katika kituo cha Stakishari siku hiyo na kutolewa tena maelezo ya nyongeza Septemba 3, 2011 na kwa mara ya tatu Septemba 21, 2011, hata hivyo hakueleza mambo yote ambayo anayaeleza mahakamani hapo.
Shahidi huyo alidai kuwa hajui kwanini lakini alitoa maelezo yote lakini aliitwa tena kutoa maelezo mengine.
Shahidi huyo akitoa ushahidi wake awali, alidai kuwa Julai 27, 2011 akiwa katika majukumu yake kama askari Magereza katika Gereza la Ukonga alipata taarifa kutoka kwa Nyampala kuwa
chumba alichokuwa akiishi Liyumba amekutwa anaongea na simu.
Awali shahidi wa kwanza Hamidu Henji (35) ambaye ni nyampala gereza la Ukonga alitoa ushahidi wake ambapo alidai kuwa siku ya tukio alimkuta Liyumba akiwa na simu sikioni, alienda kutoa taarifa kwa askari magereza na yeye kurudi katika majukumu yake.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII